GET /api/v0.1/hansard/entries/927001/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 927001,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/927001/?format=api",
    "text_counter": 247,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "pesa nyingi zilitumika. Vile vile ndugu yetu, Ken Okoth, alitumia pesa nyingi sana kujitibu. Lakini mwishowe haikuwezekana. Ni lazima liwe jukumu letu sote, kama Wakenya, kuangamiza ugonjwa huu wa saratani kwa kupitisha sheria hii ambayo italeta mageuzi mazuri, kwamba kila Mkenya aweze kufikia hospitali ili atibiwe ugonjwa huu wa saratani. Bw. Naibu Spika, mwisho naomba uniruhusu nitoe rambirambi zangu kwa familia na jamii ya Mbunge wa Kibra, ambaye alikua rafiki yangu. Urafiki wetu ulikuja baada ya kugeuziana kofia; kwa kuwa yangu ilikua inamtosha yeye, na yake ilikua inanitosha mimi. Tulikua katika zile harakati za siasa, lakini Mwenyezi Mungu ana sababu zake. Alikuwa kijana miaka 41. Aliwafanya ni mengi watu wake. Sisi sote tuliwapenda Mhe. Ken. Okoth, na dada yetu, Dkt. Joyce Laboso, lakini Mwenyezi Mungu anazo sababu zake. Ikiwa sababu za kuwachukua hawa wawili ni kuhakikisha kwamba Wakenya wote watakaobaki hai wataweza kupona, basi wao wametangulia. Ikiwa wametangulia, wametangulia kwa sababu yetu, ili vifo vyao viokoe Wakenya wote watakaopatikana na ugonjwa wa saratani ikiwa Mswada huu utapita na pia Serikali ikitia mkazo kuhakikisha kwamba hatua zimechukuliwa dhidi ya ugonjwa wa saratani. Ugonjwa huu unafaa kutangazwa kuwa janga la kitaifa ili Wakenya wote wafahamu na tuupige vita vya kutosha ili tuuangamize kabisa. Asante, Bw. Naibu Spika."
}