GET /api/v0.1/hansard/entries/927188/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 927188,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/927188/?format=api",
    "text_counter": 94,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mosop, JP",
    "speaker_title": "Hon. Vincent Tuwei",
    "speaker": {
        "id": 13436,
        "legal_name": "Vincent Kipkurui Tuwei",
        "slug": "vincent-kipkurui-tuwei"
    },
    "content": "Wiki moja iliyopita, mimi, Mhe. Serem na Mhe. Keter tulipata nafasi ya kuwazuru wakiwa hospitalini hapa Nairobi. Tulipata Mhe. Okoth na mke wake hospitalini. Tulijumuika pamoja tukiona hali ambayo alikuwa akipitia kwa uchungu wote kupitia ugonjwa huu wa saratani. Baada ya hapo, tulipata nafasi ya kumuona Gavana ambaye ametuwacha, Dr. Laboso. Sisi sote tulishtuka kuskia kwamba ametuwacha na alikuwa na imani ya kupata dawa na kupona ili arudi kufanya kazi yake ya ugavana katika kaunti ya Bomet. Lakini ya Mungu ni mengi, tumewapoteza hawa wote. Jambo la dharura ni kwamba sisi wote kama viongozi na Serikali tuchukulie saratani kama janga la kitaifa na tuweke pesa na mikakati na kutafuta mbinu na maarifa ambayo tunaweza kutumia kusaidia watu wetu."
}