GET /api/v0.1/hansard/entries/927199/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 927199,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/927199/?format=api",
    "text_counter": 105,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": {
        "id": 1612,
        "legal_name": "Bady Twalib Bady",
        "slug": "bady-twalib-bady"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika kwa kunipatia fursa hii niungane na wenzangu. Kwa niaba yangu na kwa niaba ya wananchi wote wa Jomvu, ningependa kutoa rambirambi zangu kwa wakaazi wa Kibra na Kaunti ya Bomet kwa kuwapoteza viongozi wao. Nataka kuzungumza juu ya Mhe. Ken Okoth ambaye alikuwa mtu mzuri sana. Binafsi, nilifanya kazi naye katika Bunge la 11. Mhe. Ken Okoth alikuja Jomvu kufungua madarasa huko Bangaladesh, Mikindani. Kwa hivyo, alikuwa rafiki mzuri. Mimi ni mwanakamati wa Bajeti. Miezi miwili iliyopita tulienda kushirikisha umma katika masuala ya Bajeti kule Bomet. Nilikuwa na mwenzangu, Mhe. Nyamita. Marehemu Mhe. Laboso alikuwa amekwenda hospitali. Tuliomba Mungu tukijua atampa uhai. Ingawa haya yametukia, tunasema ni kazi ya Mungu ambayo haina makosa. Kwa niaba yangu, familia yangu na wananchi wa Jomvu natoa rambirambi kwa wananchi wa Bomet na Kibra. Naomba Serikali ya Kenya itangaze saratani kuwa janga la kitaifa. Aidha, ni muhimu tuwe na hospitali za kupima saratani katika kila kaunti nchini. Nachukua nafasi hii kukushukuru Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi hii kutoa rambimbi zangu kwa familia za ndugu zetu ambao wametuacha. Asante na Mwenyezi Mungu atubariki."
}