GET /api/v0.1/hansard/entries/927393/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 927393,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/927393/?format=api",
    "text_counter": 299,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Laikipia North, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Sara Korere",
    "speaker": {
        "id": 13134,
        "legal_name": "Sara Paulata Korere",
        "slug": "sara-paulata-korere"
    },
    "content": " Ninakushukuru Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi niweze kuchangia suala hili. Ni suala nyeti. Ninataka pia kumpongeza mwenzangu Mbunge wa Turkana Mashariki kwa kuileta Hoja hii. Ninakotoka, anakotoka yeye na wanakotoka baadhi yetu hapa wafugaji tumekuwa waathiriwa wakubwa sana katika suala hili la kupokonywa polisi wa ziada, almaarufu NPR. Alivyonena yule alitangulia kuwasilisha suala hili ni kwamba wizi wa mifugo katika nchi hii na haswa katika maeneo tunakotoka sisi wafugaji imekuwa biashara ambayo iko na wenyewe. Kila siku tunapojaribu kutatua suala hili, majibu tunayopata kutoka kwa wale ambao tumewapatia vifaa vya kulinda usalama wetu ni kwamba wanawajua na watawakamata. Wakati hawakamatwi, tunaendelea kupoteza maisha ya binadamu na mali ya wananchi ambao tunawakilisha katika Bunge hili. Tunaendelea kuona shule zikifungwa kwa sababu ya ukosefu wa usalama. Katiba ya nchi hii inasema kwamba usalama wa mali na uhai wa binadamu ni suala la kikatiba. Kwa hivyo, tukirejelea masuala hayo, wale wananchi wa kaunti za Turkana, Laikipia na Baringo, haki yao ya kikatiba ya usalama na usalama wa mali yao imekiukwa na Serikali ya nchi hii. Tulipokuwa na Inspekta Mkuu wa Polisi ambaye aliondoka afisi hivi majuzi, Bw. Boinnet, aliweza kutambua mahali ambapo kulihitajika usalama katika nchi hii na wakaweza kuwahamisha wale askari wa ziada, ambao ni vijana kutoka jamii hizo ili waweze kudhibiti wizi wa mifugo na ushambulizi wa majambazi ambao wamejihami kwa silaha hatari. Mimi ni mmoja The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}