GET /api/v0.1/hansard/entries/927394/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 927394,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/927394/?format=api",
    "text_counter": 300,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Laikipia North, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Sara Korere",
    "speaker": {
        "id": 13134,
        "legal_name": "Sara Paulata Korere",
        "slug": "sara-paulata-korere"
    },
    "content": "wa waathiriwa, maanake Laikipia Kaskazini tumepoteza mali nyingi sana, haswa kuanzia mwaka wa 2013 hadi 2017 wakati tulipewa hawa polisi wa ziada. Wabunge wenzangu watakubaliana na mimi kuwa wakati tulipata hawa askari wa ziada, shida zetu zilipungua kwa kiasi cha haja. Awali, mali zetu zikiibiwa na hawa majambazi ambao wamejihami kwa silaha hatari, polisi wa kawaida… Tunajua, na sio siri, vile uajiri unaendelea katika nchi hii. Unamtoa mtoto Nairobi, hajawahi kanyaga Turkana, unampeleka kule. Akifuata hiyo mali kilomita moja anarudi kwa kambi. Hawa askari wa ziada wanafuata mali zetu kwenye mabonde na milima mpaka wanahakikisha zimerudi. Pia, usalama wa raia wa kawaida unaimarishwa sana wakati wale askari wa ziada wako katika maboma zetu. Baadhi ya visingizio ambavyo tunapewa na wale ambao wanasimamia idara ya usalama ni kwamba kuna baadhi ya wale askari wa ziada ambao wanatumia hizo silaha vibaya. Tunajua kuna polisi wa kawaida ambao wamejiua wakitumia hizo silaha. Wengine wameua wake zao, marafiki zao na pia raia. Lakini hatujasikia yule Waziri ambaye anahusika na usalama akisema polisi wote wapokonywe silaha. Kwa hivyo, mimi ninarai na kusihi Bunge hili kwamba maneno ya watu kukula mandazi Nairobi na kutoa amri kwa mahali ambayo hawana…"
}