GET /api/v0.1/hansard/entries/927415/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 927415,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/927415/?format=api",
    "text_counter": 321,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Baringo South, JP",
    "speaker_title": "Hon. Charles Kamuren",
    "speaker": {
        "id": 1202,
        "legal_name": "Charles Kamuren",
        "slug": "charles-kamuren"
    },
    "content": " Ninasimama kuunga mkono mjadala huu kuhusu amani. Wakaaji wa eneo langu la Baringo Kusini wamepoteza maisha kwa ajili ya mambo ya wizi wa ng’ombe. Hawa sio wezi wa ng’ombe lakini ukora unaojulikana na biashara kwa wengine. Ninakubaliana na wengine kwamba Serikali inajua wale ambao wanafaidika na biashara ya wizi wa ng’ombe. Wanaelewa kazi yao na kuna ukora. Inaonekana kwamba kuna wafanyakazi wa Serikali ambao wanakulia jambo hili. Huu ni ufisadi mwingine nchini humu na ni mbaya kwa sababu hawa wakora wanawaua watu wetu. Katika eneo langu la Baringo Kusini, tumepoteza maisha ya watu 278 kufikia sasa. Mwaka uliopita, waliua watoto watano ambao walikuwa wanasoma na wakachukua ng’ombe. Juzi tena, wakamuua mwanafunzi. Jumatatu wiki iliyopita, tulikuwa kwenye mazishi. Wamechukua ng’ombe katika sehemu za Arabal, Mukutani na Rugus. Inajulikana vizuri na ukiuliza Serikali, inasema kwamba wanawajua hao. Kama wenye The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}