GET /api/v0.1/hansard/entries/927417/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 927417,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/927417/?format=api",
"text_counter": 323,
"type": "speech",
"speaker_name": "Baringo South, JP",
"speaker_title": "Hon. Charles Kamuren",
"speaker": {
"id": 1202,
"legal_name": "Charles Kamuren",
"slug": "charles-kamuren"
},
"content": "Ninamuomba Rais wetu, Uhuru, ajue kwamba watu wengine tunaishi katika ufukara na umaskini na tunapoteza maisha yetu. Shule 11 zilifungwa katika eneo bunge langu. Hivi majuzi, tulifungua shule zingine na zingine bado zinafungwa. Wanaiba mchana kwa sababu bunduki ambazo zilichukuliwa na polisi wa ziada zilirudishwa. Sasa wanakuja saa tisa au saa sita mchana na kuwaua watu wetu. Serikali inajua. Tunaambiwa helicopter inakuja lakini maisha yamepotea. Tumebaki na wale ambao wako hospitalini na tunachanga pesa ili tugharamie malipo ya hospitali. Hili ni jambo mbaya katika nchi hii. Ninaomba yule ambaye alichukua Biblia na kusema kwamba atachunga mali na maisha ya wananchi kwamba hukumu iko mbele yake kwa sababu hatuwezi kuwa tukilia katika nchi hii wakati wengine wanakaa vizuri."
}