GET /api/v0.1/hansard/entries/92756/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 92756,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/92756/?format=api",
"text_counter": 119,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ms. Leshomo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, ningependa kumshukuru Waziri Msaidizi kwa kutueleza kwamba hakuna watu wametengwa kuhusiana na vitambulisho. Ni muhimu Wakenya wawe na vitambulisho. Katika maeneo kama hayo utamkuta mtu ana umri wa miaka 60 lakini hana kitambulisho. Pia, watu wengi hutembea kilomita 70 kutafuta kitambulisho, kwa mfano, kutoka Baragoi hadi Maralal kwa sababu hakuna magari ya kusafirisha. Utafika huko namna gani? Katika harakati zangu za kutafuta amani, nimekutana na vijana wengi ambao hawana vitambulisho. Huu muda wote tumelia kwamba watu wetu hawana vitambulisho, je, Waziri Msaidizi anaweza kutueleza ina maana gani kusemekana kwamba sharti kila Mkenya awe na kitambulisho ilhali Serikali haitilii maanani watu kuwa na vitambulisho? Anafaa kutujulisha kwa njia bora ili tujue. Katika maeneo hayo, watu wanasema kwamba wao si Wakenya kwa sababu hawana vitambulisho. Ningependa kumwuliza Waziri Msaidizi atujulishe kwa njia ya ukweli."
}