GET /api/v0.1/hansard/entries/92757/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 92757,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/92757/?format=api",
"text_counter": 120,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Baya",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 10,
"legal_name": "Francis S. K. Baya",
"slug": "francis-baya"
},
"content": "Bw. Naibu Spika maelezo yamekuwa mengi mpaka maswali yamepotea. Hata hivyo, ningependa kumwunga mkono mhe. Leshomo kwamba sehemu kame, kwa sababu ya ukubwa wake, wananchi kwa kweli wana shida kupata vitambulisho. Lakini kama nilivyosema hapo awali ni kwamba tumetoa fomu hadi tarafa. Siku hizi tarafa ziko karibu sana na wananchi. Kutoka Januari, 2010 hadi Juni, 2010, tumeandikisha watu 2,975 huko Samburu. Kati ya watu hawa, tuna vitambulisho 616 ambavyo havijachukuliwa. Kwa hivyo, tunamwomba mhe. Leshomo atusaidie kwa kuwauliza wale ambao hawajachukuwa vitambulisho vyao kufanya hivyo."
}