GET /api/v0.1/hansard/entries/92770/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 92770,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/92770/?format=api",
"text_counter": 133,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Ethuro",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 158,
"legal_name": "Ekwee David Ethuro",
"slug": "ekwee-ethuro"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, hili Swali ni la maana sana na Wizara hii ni ya Uhamiaji na Usajili wa Watu. Je, watu kutoka jamii zilizotengwa ambao hawajasajiliwa watapata vitambulisho lini? Je, Waziri Msaidizi ameweka hatua gani kabambe kuhakikisha kuwa watapata vitambulisho hivyo? Sasa hivi kwangu kule, Turkana ya Kati, upande wa Kangâirisae, machifu wameandikisha watu 500 na wanawangoja maofisa wa usajili waende kusajili watu. Katika Napeilelim na Namorupus karibu 5,000 hawana vitambulisho ilhali ni haki ya Mkenya kupata kitambulisho. Kwa maoni yangu, Waziri Msaidizi hajajibu hili Swali kabisa kwa sababu hajatupatia mpango kabambe ambao Serikali imeweka kuhakikisha ya kwamba watu wote wamepata huduma ambayo ni haki yao kama Wakenya. Ningependa Swali hili liahirishwe mpaka Waziri Msaidizi aje na mpango kabambe."
}