GET /api/v0.1/hansard/entries/92772/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 92772,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/92772/?format=api",
"text_counter": 135,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Baya",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 10,
"legal_name": "Francis S. K. Baya",
"slug": "francis-baya"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, Swali lililoulizwa na mhe. Mbunge kama Wizara tumejaribu kulijibu. Lakini kuna sehemu ambazo pengine ziko na shida maalum. Nimesema ya kwamba tumeomba pesa ili tuongeze magari na mafuta. Pia, tunatumia maafisa wa utawala na hata walimu wakuu kuhakikisha kwamba tunawasajili wale ambao hawajapata vitambulisho kwa haraka iwezekanavyo. Kwa hivyo, kama Turkana ambayo naifahamu sana iko na shida hiyo, nafikiri itabidi kuongeza maofisa. Nikirudi ofisini, nitafanya mpango maalum ili tupeleke maofisa zaidi ili hao mamia ya watu ambao wako huko wasajiliwe."
}