GET /api/v0.1/hansard/entries/92776/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 92776,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/92776/?format=api",
    "text_counter": 139,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ms Leshomo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, inaonekana kwamba kuna shida katika shughuli za kuwasajili watu wetu ili wapate vitambulisho. Ningeomba Waziri Msaidizi ajaribu kuzipatia nguvu idara ambazo ziko kwa wilaya ili kila mtu apate kitambulisho. Naibu Waziri angetueleza vile tunaweza kupata idara ambayo ni mobile ambayo inaweza kuzunguka katika kila kata ili kuwasajili watu. Tukiuliza Swali na mambo hayo hayatekelezwi, haisaidii. Ningeomba Idara ya Usajili wa Watu iimarishwe. Hii ni kwa sababu utapata mtoto anashtakiwa kwa kukosa kitambulisho. Je, ni nini itaonyesha kuwa yeye ni Mkenya kama hana kitambulisho? Kwa hivyo Idara ya Usajili wa Watu ingefanya juhudi zaidi kuhakikisha kuwa Wakenya wote wanapata vitambulisho. Pia tuwe na ofisi ambazo ni mobile . Pia, itachangia katika kuimarisha hali ya usalama."
}