GET /api/v0.1/hansard/entries/928927/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 928927,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/928927/?format=api",
"text_counter": 199,
"type": "speech",
"speaker_name": "Trans Nzoia CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Janet Nangabo",
"speaker": {
"id": 1076,
"legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
"slug": "janet-nangabo-wanyama"
},
"content": " Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nichangie Mswada huu ulioletwa na Mbunge wangu wa Kiminini. Huu ni Mswada unaoenda kurekebisha mambo katika nchi yetu ya Kenya. Kabla sijaendelea, nachukua fursa hii kutuma rambirambi zangu pamoja na za watu wa Trans Nzoia, kwa familia za wenzetu waliopoteza maisha yao, Gavana Joyce Laboso na ndugu yetu Ken kutoka Kibra. Walikuwa viongozi waliochangia mengi sana katika nchi yetu ya Kenya. Walioonyesha msimamo wao hata wakati wa siasa bila kuegemea upande wowote. Mhe. Naibu Spika wa Muda, nikubalie niongee kuhusu Mswada huu ulioletwa na Mhe. Chris Wamalwa kuhusu wakurugenzi katika taasisi mbalimbali katika nchi yetu ya Kenya. Vile wenzangu wamesema ni kweli. Tumekuwa na wakurugenzi katika kampuni na taasisi tofauti katika nchi yetu ya Kenya ambao wamenyanyasa watu. Nakumatt Supermarket ilianguka kwa sababu tulikuwa na wakurugenzi ambao hawakujua kazi yao ilhali hakuna mtu aliyejali kuchunguza kilichokuwa kinaendelea katika kampuni hiyo. Ndiyo maana nasema ni vizuri sana tuwe na wakurugenzi katika taasisi hizi kwa sababu watakuwa wanachunguza mambo yanavyoendelea katika taasisi ambazo wanashirikiana nazo."
}