GET /api/v0.1/hansard/entries/928930/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 928930,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/928930/?format=api",
"text_counter": 202,
"type": "speech",
"speaker_name": "Trans Nzoia CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Janet Nangabo",
"speaker": {
"id": 1076,
"legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
"slug": "janet-nangabo-wanyama"
},
"content": "Kile kimenifurahisha ni washikadau hao watakuwa wanahudumu kwa miaka mitatu tu na baada ya miaka mitatu, huenda ikawa tutakuwa na wengine. Hivyo ni vizuri sana kwa sababu mtu akifanya kazi atakuwa anajichunguza jinsi alivyo na jinsi anavyoendesha mambo yake. Wengine wasipokuwa na nidhamu katika kazi zao lazima wachukuliwe hatua kwa sababu haitakuwa vyema mtu kukosea halafu aende bure bila mkono wa sheria kuchukua mkondo wake. Ninawaomba wale watapata nafasi kushirikiana na wengine katika taasisi mbalimbali wawe watu wa nidhamu na waelewe kazi yao. Tumegadhabishwa sana na serikali za kaunti. Nyingi zimeharibu pesa na hazijafanya kazi nzuri. Ndiposa wanasema kwamba taasisi hii inatakikana kuchukuliwe na mtu aliye na maadili mazuri hata kama amefanya kazi kwingine na kuingia kwingine. Hiyo itahakikisha kwamba akipewa nafasi ya kuhudumu katika taasisi hii atakuwa mtu aliye na nidhamu na sio mtu aliyeharibu kwingine na kwa sababu ya siasa, anachukuliwa tu mara moja na kupewa nafasi tena katika taasisi ingine. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}