GET /api/v0.1/hansard/entries/929077/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 929077,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/929077/?format=api",
    "text_counter": 70,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa ya kuendelea. Hili ombi limechukua mkondo fulani tayari. Ni vizuri watu ambao wamejitoa mhanga kulinda nchi na mipaka yetu wapewe heshima. Jambo la kushangaza ni kwamba wanajeshi waliostaafu wanaishi maisha ya uchochole na familia zao ilhali walijitoa mhanga kutulinda. Ule mwelekeo ulioko sasa ni kwamba, kuwekwe sheria ya kuwapa bima na fidia ya kutosha, kwa sababu wengine wao walitoka na madhara ya kimwili na kiakili. Kwa hivyo, sheria itungwe ya kuwafidia watu hawa Wanajeshi hawa ambao wamestaafu wana watoto, mabibi, familia na maisha baada ya Huduma yao---"
}