GET /api/v0.1/hansard/entries/929093/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 929093,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/929093/?format=api",
"text_counter": 86,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Mhe. Spika, kwa kunipa fursa hii. Ninataka kuchangia maombi ya mhe. Khaniri ya kutaka maaskari wakongwe kuangaliwa. Tatizo la maaskari wakongwe halijaanza sasa. Lilianza na serikali ya ukoloni. Serikali ya ukoloni iliwachukua ndugu zetu wengi na ikawapeleka India, Burma na kwengineko kupigana vita. Waliporudishwa nyumbani walipewa pesa duni kama malipo ya uzeeni. Waafrika walilipwa tofauti na Wahindi na Wazungu, ilhali walipigana vitu pamoja. Tatizo hili halikuanza na Serikali hii. Lilianza na Serikali ya ukoloni. Serikali ya ukoloni haikudhamini maisha ya Waafrika. Askari wetu wa Kenya wako katika vita kule Somalia na wakimaliza kandarasi yao, wao hupewa malipo duni ambayo hayatawawezesha kuishi maisha mazuri. Kwa hivyo, maombi haya yameletwa katika wakati mwafaka. Tunapoendelea, tunaona ya kwamba matatizo ya askari wakongwe yanazidi kuongezeka. Kwa mfano, wengi wao wanapata majinamizi usiku kwa sababu walipokuwa kwenye vita walipata madhara."
}