GET /api/v0.1/hansard/entries/92928/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 92928,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/92928/?format=api",
"text_counter": 291,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwatela",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Education",
"speaker": {
"id": 103,
"legal_name": "Andrew Calist Mwatela",
"slug": "andrew-mwatela"
},
"content": " Asante, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Ningependa kutofautiana kidogo na ndugu yangu, mhe. Shabeel, kuwa Wizara hii ingekuwa moja. Ninaona ni vizuri Wizara hizi ziendelee kuwa tofauti. Kwanza, ninaunga mkono kazi inayofanywa na Waziri pamoja na kikosi chake kuhakikisha kuwa wananchi wanaendelea kuwa na afya bora. Kazi muhimu ya Wizara hii ni ya kuzuia maradhi na kuhakikikisha kuwa wananchi wetu wako na afya nzuri. Ni tofauti sana na kazi ya kutibu watu. Ingekuwa ni Wizara ambayo inaunganiza Wizara nyingi za Serikali mojawapo ikiwa Wizara ya Maji na Unyunyizaji, Wizara ya Elimu na Wizara ya Ardhi. Kuna sehemu ambazo zinalimwa na watu ambazo zinahatarisha ama kuruhusu kuchafuka kwa maji. Kama hatua zingechukuliwa kuhakikisha kuwa sehemu hizo hazilimwi, bila shaka sehemu hizo zingekuwa na maji safi zaidi. Naendelea kumshukuru Waziri kwa namna ya kipekee kwa sababu mara nyingi nimefika kwake kumwomba mizaada tofauti ya dharura. Hata leo hivi, amenipatia msaada kidogo kwa sababu ni na kambi ya kujaribu kuhudumia watu wangu Jumamosi hii. Ninamwalika ndugu aje kushuhudia jinsi tunavyowahudumia wagojwa. Nakushukuru Waziri kwa kazi yake nzuri. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}