GET /api/v0.1/hansard/entries/930378/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 930378,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/930378/?format=api",
"text_counter": 95,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lungalunga, JP",
"speaker_title": "Hon. Khatib Mwashetani",
"speaker": {
"id": 2163,
"legal_name": "Khatib Abdallah Mwashetani",
"slug": "khatib-abdallah-mwashetani"
},
"content": " Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii. Hili ni jambo ambalo ni sugu sana. Kusema kweli, dakika 15 zitakuwa chache sana. Hivi tunavyozungumza, kuja kwa SGR ni maendeleo lakini sasa hivi, kulingana na maelekezo kuwa kasha lolote linalokuja lazima libebwe na SGR mbali na lile kasha ambalo latakikana libakie Mombasa, watu wengi wamefunga maduka. Ukiangalia barabara ya kutoka Nairobi hadi Mombasa, kumekuwa na vitongoji na vijiji kadhaa wa kadhaa ambavyo miaka yote viko na shughuli nyingi. Lakini kutoka shughuli hii ianze, kazi zote zimekufa. Haya si makosa yetu. Kazi ya SGR ilipofanywa, mategemeo ni kuwa ilikuwa ijilipe yenyewe. Lakini kulingana na mipango ile ipo, imeshindwa kujilipa. Haiwezi kulazimisha wawekezaji waingie katika hasara ya kupoteza pesa. Wengine wamechukua pesa katika mabenki. Naomba hili suala lipewe muda mrefu kama vile wenzangu walizungumza ili tuweze kulichangia kisawasawa. Ahsante."
}