GET /api/v0.1/hansard/entries/930453/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 930453,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/930453/?format=api",
    "text_counter": 170,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Bura, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Wario",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": " Ahsante, Mheshimiwa Naibu Spika kwa kunipa fursa hii niweze kuunga mkono Kiongozi wa Walio Wengi katika Bunge kwa Mswada aliyoleta Bungeni siku ya leo. Mswada wa Halmashauri ya Kuchunguza Hali ya Ukame ulisomwa mara ya kwanza tarehe 2/5/2019. Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, mia mbili kumi na sita (g) wajibu wa kusimamia halmashauri hii uko chini ya Kamati ya Utendakazi na Ustawi. Leo nimepata fursa ya kuweza kuunga mkono Kiongozi wa Walio Wengi katika Bunge. Mswada huu umeletwa kwetu baada ya Karani wa Bunge kutangaza magazetini na Wakenya wengi kuleta maoni yao. Katika maoni hayo, wengi wameunga mkono pendekezo lililoletwa mbele ya Bunge."
}