GET /api/v0.1/hansard/entries/930457/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 930457,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/930457/?format=api",
"text_counter": 174,
"type": "speech",
"speaker_name": "Bura, JP",
"speaker_title": "Hon. Ali Wario",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Kabla sijakaa chini, ningependa kusema kwamba ninatoka Tana River na upande wa Tana North, kuna ukame mkubwa. Upande wa Garsen South na Lamu kunanyesha mvua. Wengi wa wafugaji wamelazimika, kwa sababu ya ukame, watoke Tana North, Bura an Galole waelekee upande wa Lamu na Garsen. Idadi ya wafugaji walioteremka huko ni kubwa. Kufuatia jambo hili kukawa na mzozo baina ya wenye mashamba na wenye mifugo. Kwa bahati mbaya, walinda usalama, badala ya kutatua mzozo uliotokea na kuchukua hatua, wanachoma nyumba za wafugaji na kupiga watu kiholela bila kuangalia haki na sheria ya taifa. Nalaani vikali tendo hilo! Taifa na watunzi wa sheria wanastahili kutambua ufugaji. Mifugo ni rasilimali ya taifa."
}