GET /api/v0.1/hansard/entries/930541/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 930541,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/930541/?format=api",
"text_counter": 258,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": "kama sehemu ambazo mvua hunyesha lakini sehemu kama Kiunga hakunyeshi. Watu wa Kiunga si wavivu, ni watu wa kwenda mashambani kulima. Hata hivyo, hawawezi kwenda kwa mashamba kwa sababu ya utovu wa usalama. Watu kama hawa watafanywa vipi? Sehemu ya Kiunga ni sehemu ya oparesheni. Sehemu za Kiunga na Basuba Ward ambazo ziko Lamu East, na upande wa Hindi Witu, watu wa Lamu wanapata shida. Tumelalamika kwamba mashamba yako na mvua, ipo lakini hatuwezi kwenda kulima. Kuna watu kutoka Basuba Ward ambao wameenda Kiunga. Wamekaa huko na wanawasomesha watoto wao huko. Halmashauri kama hii inafaa iwafikirie watu kama hawa. Witu imekuwa kambi kwa muda kwa sababu watu hawawezi kwenda kulima. Naomba Lamu izingatiwe kwa sababu haikujumuishwa katika miradi yao. Tunaomba wazingatie watu wa Lamu kwa sababu wanaumia na hawana chakula. Wanataka kufanya kazi lakini kazi hazifanyiki. Wakienda mashambani, maafisa wa Kenya Defence Forces (KDF) wanawapiga. Ni lazima itafutwe njia hata kama ni alama au kitambulisho, wapewe ili wajulikane ni wakaazi tofauti na wahalifu ili waende wakalime. Kama haiwezekani kufanya hivyo, halmashauri hii ihakikishe watu wamepewa chakula cha kutosha kukidhi mahitaji yao ili wasiende mashambani. Ahsante. Sina mengi. Naunga mkono Mswada."
}