GET /api/v0.1/hansard/entries/930543/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 930543,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/930543/?format=api",
    "text_counter": 260,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": {
        "id": 1612,
        "legal_name": "Bady Twalib Bady",
        "slug": "bady-twalib-bady"
    },
    "content": " Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia hii nafasi ili niweze kuunga mkono Mswada huu ambao haswa ni Mswada No. 26 wa mwaka 2019 na unaosomwa kwa Mara ya Pili. Juu ya jambo kama hili pia mimi naunga mkono viongozi wenzangu, akiwemo Mhe. Ruweida Obo ambaye amezungumza sasa hivi juu ya shida za Lamu. Vile vile, naunga mkono kwa sababu Lamu na Mombasa siyo mbali. Naamini ni kweli kuwa pia wao wawekwe katika hazina hii ili waweze kusaidiwa kama watu wengine ambao wanasaidiwa. Leo ni jambo la kutamausha sana kuwa kutoka Kenya ipate Uhuru mpaka leo, ni miaka mingi sana ilhali bado tunazungumzia suala la ukame. Lakini juu ya yote nataka kuunga mkono Mswada huu kwa sababu wakati huu wetu ambapo sisi ndio viongozi, tunashukuru kwa maana halmashauri hii ya kupambana na makali ya ukame itaweza kufanya kazi kikamilifu kulingana na yale mapendekezo ambayo wametoa. Jambo la muhimu sana ambalo nimeweza kuliona katika Mswada huu ni kuletwa kwa zile fedha ambazo itabidi ziweze kuangalia makali ya ukame ambayo yatakuwa yanakumba sehemu mbalimbali katika nchi yetu ya Kenya. Kwa hivyo, hata mimi naungana na wenzangu wengi sana ambao walisema kuwa kaunti zao pia ziweze kuangaliwa na kuwekwa kati ya zile ambazo zaweza kufikiriwa kupata manufaa kupitia hazina hii. Kwa maana hiyo, nasema Kaunti ya Mombasa, ambapo ninatoka, pia ni muhimu kuangaliwa katika hazina hii ili nasi tufaidike. Namwona Mhe. Obo pale hafurahi kwa sababu watu wengi waliozungumza hapa kutoka Kirinyaga, Turkana, Kitui, Machakos, Makueni na sehemu mbali mbali, wanachukulia kwamba makali haya yatawaathiri wao pekee yao ambao wanafanya ukulima. Lakini mimi na wewe Mhe. Naibu Spika wa Muda, tumekuwa pale Mombasa na tukatembea sehemu mbali mbali za Mombasa hasa kwenye mahoteli makubwa makubwa na majumba ambamo watu wanakula kamba, ambacho ni chakula kizuri sana. Chakula hiki hakiwezi kupatikana baharini bila kuwepo mikondo ya mito kuelekea baharini. Kamba huzaana kwa wingi kwenye hiyo mikondo. Kwa hivyo, mkondo huu hauwezi kuwepo ikiwa kiwango cha maji kitakuwa chini. Na kiwango cha maji kuwa chini hakiwezi kuletwa hivi hivi isipokuwa kitaletwa na kiangazi. Kwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}