GET /api/v0.1/hansard/entries/930544/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 930544,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/930544/?format=api",
    "text_counter": 261,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": {
        "id": 1612,
        "legal_name": "Bady Twalib Bady",
        "slug": "bady-twalib-bady"
    },
    "content": "hivyo, kitaalamu, nimezungumzia jambo hili ili kujitetea kuwa sisi watu wa Mombasa huenda ukulima wetu sio sana wa kushika jembe lakini ukulima wetu pia ni ile bahari na wale viumbe ambao wanapatikana katika bahari. Kwa hivyo, naona ni muhimu zaidi Serikali kuu inapoangazia mambo haya, kaunti yangu ya Mombasa nayo ifaidike. Jambo la pili ambalo nataka kulisema ni kuwa viwango vya maji vikiwa chini huwa ni sababu ya ukame. Ni huo ukame unaosababisha watu kukosa maji ya kunywa. Leo hii nikizungumza hapa, kuna shida kubwa ya ukosefu wa maji ya kunywa Mombasa. Hii ni kwa sababu maji ambayo yanatumika katika sehemu za Mombasa yanatoka Mzima Springs na Marere. Ukame unapozidi, viwango vya maji huwa chini na watu hupata shida. Lakini kulingana na hazina hii, kuna utaalamu ambao unaweza kufanyika. Nasema hivi kwa sababu kule Pwani kuna sehemu inayoitwa Mtwapa ambapo kuna Mjerumani anayetengeneza maji mazuri kutokamana na maji ya bahari. Maji yale yanaitwa Dutch Water. Maji yale ndiyo wengi wanatumia katika nyumba zao na kwa njia tofauti tofauti. Kwa hivyo fedha hizi zikitumiwa vizuri… Ikiwa mwekezaji mmoja ameweza kujiletea faida katika bishara yake, kwa nini pesa hizi zisitumiwe na Serikali ili kuwawezesha wananchi wa Pwani kuishi wakiwa na maji safi katika nyumba zao? Sharti kila mmoja apate haki hii ambayo ni ya kisheria kulingana na Katiba. Tulipopata Uhuru katika nchi yetu tulisema tunataka tuondoe umaskini, baa la njaa, na matatizo ya vitu muhimu kama hivi ambavyo vinastahili kutumika. Naamini ikiwa fedha hizi zitafanyiwa mipango mizuri basi zitaweza kutumika na hali Mombasa mjini na hata Jomvu ninakoongoza itaimarika. Taaluma hii ikifanyika, wananchi watasaidika. Kule Mikindani kuna mkondo wa bahari. Miritini, kuna mkondo wa bahari katika sehemu inayoitwa Mkupe. Jomvu Kuu, kuna mkondo wa bahari Jomvu Kuu yenyewe na Misheni. Kwa hivyo, taaluma hii itawasaidia wananchi wetu pakubwa. Amesema hapa Mhe. Sophia kuwa pesa zatumika nyingi sana, karibu KSh8 bilioni ama hata kuzidi. Wakati matatizo yanapotokea ndipo utaona watu wakikimbilia Red Cross, World Vision na mashirika mengine yasiyo ya Serikali. Serikali ambayo ina uhuru kamili na inajali maslahi ya watu wake ni serikali ya kujipanga. Kwa hivyo, hivi sasa tunasema kuwa kuundwa kwa halmashauri hii na kuwekwa pesa za kudhibiti makali ya ukame… Tunatumai mambo haya yatasimamiwa vizuri. Kabla matatizo hayajatokea watu huwa na mipango mizuri. Huwa kuna fedha zakutumika kusaidia waathiriwa. Kwa hivyo, naunga mkono mapendekezo haya. Vile vile, katika mapendekezo haya, tumeunga mkono kuwa kuwekwe pesa ambazo zitasimamiwa na halmashauri hii. Lakini vile vile nasema, na nataka ninukuliwe katika Bunge hili, kuwa pesa hizi lazima zitumiwe kwa njia ambayo ni ya sawasawa na sio sisi tuidhinishe pesa hapa kumbe tunawawekea watu wengine pesa hizo kula badala ya kusaidia wananchi wa Kenya katika masuala yale. Kwa hivyo, viongozi ambao watasimamia halmashauri hii lazima wawe waadilifu na watumikie Wakenya. Wajue Wakenya wote wako na haki ya kuishi vizuri. Kwa hayo, asante kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia. Naunga mkono mapendekezo haya. Asante sana na Mungu atubariki."
}