GET /api/v0.1/hansard/entries/930575/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 930575,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/930575/?format=api",
"text_counter": 292,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kaloleni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Paul Katana",
"speaker": {
"id": 13357,
"legal_name": "Paul Kahindi Katana",
"slug": "paul-kahindi-katana-2"
},
"content": " Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii. Nimesimama kuunga mkono Mswada huu. Hakuna nchi ambayo inaweza kuendelea kiuchumi, kisiasa na kijamii kama watu wake wana njaa. Ni jambo la kusikitisha kwamba baada ya zaidi ya miaka 50 ya Uhuru, watu wetu bado wanategemea chakula cha msaada. Ukame unaathiri watu wengi kwa sababu Serikali haijakuwa na mipango maalum ya kupambana na ukame ili usiwaumize watu wetu. Hii ni kwa sababu hatujatumia viwango ambavyo tunapatiwa na wizara inayohusika na mambo ya hali ya hewa. Wakati kuna baridi, watu hujipanga kununua nguo ambazo zinakinga baridi na wakati wa joto, watu wanapanga kununua nguo za joto. Kwa nini hatuwezi kujipanga tujue ni wakati gani kutakuwa na kiangazi na wakati gani kutakuwa na chakula cha kutosha? Mvua imenyesha takriban miezi miwili iliyopita. Kwa nini wakati huu kuna njaa? Hii ni kwa sababu maji yote ambayo yangekingwa na kutumika baadaye yameenda baharini. Katika Eneo Bunge langu la Kaloleni, sehemu za Ndatani na Mwanamwinga, saa hii kuna ukame na watu wanategemea chakula cha msaada. Ukame huu pia umefanya wanyamapori kutoka sehemu za Tsavo na kuingia Mariakani na Ndatani na kuwasumbua wananchi. Hii ni kwa sababu Serikali haina mipango maalum ya kuhakikisha kwamba wananchi hawahangaiki kutokana na mambo ya chakula. Kenya inapata mvua mara mbili kwa mwaka. Lakini angalia nchi ambazo ziko kwa jangwa kama Israel. Wakati tulienda Israel, tulikuta kwamba inatoa chakula kingi kushida Kenya kwa sababu wamejipanga njia gani watatumia ili wananchi wake wasiathirike."
}