GET /api/v0.1/hansard/entries/930576/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 930576,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/930576/?format=api",
    "text_counter": 293,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kaloleni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Paul Katana",
    "speaker": {
        "id": 13357,
        "legal_name": "Paul Kahindi Katana",
        "slug": "paul-kahindi-katana-2"
    },
    "content": "Ninaunga mkono Mswada huu lakini ni lazima kuwe na mipango maalum. Pesa ambazo zitawekwa katika hazina hii zitumike ili tujipange. Tusingoje mpaka watu waumie ama wakufe kwa sababu ya njaa ndio tuanze kutafuta pesa na misaada kutoka nchi za nje. Inatakikana tujipange mapema ili tuweze kuokoa watu wetu. Wakati mwingi watu wanakufa kwa sababu ya njaa halafu Serikali inakataa. Hii ni hali ambayo ipo. Serikali inatakikana ijitokeze, ishirikishe watu wote ambao wanahusika, haswa viongozi kutoka kule chini mashinani, ili tuweze kujua ni njia gani tunaweza kuweka mipango maalum ili tusaidie watu wetu."
}