GET /api/v0.1/hansard/entries/930626/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 930626,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/930626/?format=api",
    "text_counter": 343,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": " Asante sana Naibu Spika wa Muda. Hata mimi nasimama kuunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na Mbunge mwenzangu kutoka Mvita kuzungumzia mambo ya uchukuzi wa shehena ama makasha katika bandari yetu ya Mombasa. Nazungumzia suala hili kwa sababu agizo hili ambalo limetolewa kwamba kila kasha, shehena ama mizigo ambayo itaingia poti itumie reli ni jambo ambalo litaathiri uchumi, haswa wa sehemu ya Mombasa, Pwani na hata Kenya kwa jumla. Tunajua kwamba wakati wafanyibiashara wanaleta mizigo ama mali kutoka sehemu tofauti tofauti, mali hii huwa si ya Nairobi peke yake. Mali nyingine ni ya Mombasa, nyingine ni ya Voi na sehemu zingine za nchi yetu ya Kenya, kabla kufika Nairobi. Kwa hivyo, iwapo mtu atalazimishwa mizigo ifike Nairobi tena irudi Mombasa, hizo ni gharama mara ya pili. Jambo la pili, tunazungumzia kujenga ajira. Agizo hili linazungumzia kumaliza ajira zilizoko hivi sasa. Tunajua mambo ya uchukuzi yamejenga ajira kwa vijana wengi sana. Mambo ya CFSs, ya clearing and forwarding na mambo mengi ambayo yanafanyika katika bandari yetu yanapeana ajira nyingi sana kwa vijana wetu. Itakuwaje tunazungumzia kujenga ajira na huku tunavunja ajira zilizoko? Vilevile, tuulize, SGR iliyoko ina uwezo wa kubeba ile mizigo ama yale makasha yote yanayoingia katika bandari ya Mombasa kwa wakati unaofaa? Ni lazima tuangalie wakati katika biashara. Wakati ukipotea, uchumi unapoteza na pia faida nyingi imepotea. Kwa hivyo, iwapo tunataka kutengeneza maamuzi ya kutoa agizo lolote, lazima kwanza tuangalie faida na hasara zake ni gani. Tunajua kuna changamoto katika mambo ya SGR. Iwapo changamoto hii itafanyika au kutatuliwa kwa njia ya kuumiza Wakenya wengi, hili ni jambo ambalo halifai. Kwa hivyo, agizo hilo si sawa na hatutaliunga mkono. Sisi viongozi tunakemea sana agizo hili. Kwa sababu soko la Kenya ni soko huru, tunataka uamuzi."
}