GET /api/v0.1/hansard/entries/930644/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 930644,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/930644/?format=api",
"text_counter": 361,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": " Asante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili niweze kuchangia Hoja hii ilioletwa na ndugu yangu, Mhe. Sherrif Nassir. Nataka kuipinga vikali sana ile amri inayosema kuwa makasha yote yanayotoka katika bandari ya Mombasa yabebwe kupitia SGR hadi Embakasi. Kenya ni nchi huru na kila mfanyibiashara ana haki ya kuamua makasha yake yachukuliwe barabarani ama kwenye reli kupitia SGR. Kitu ambacho ninazungumzia ni muhimu sana. Serikali ya Kenya lazima iweze kusawazisha. Kuja kwa mradi wa SGR kusiwe ndio kifo cha makampuni yetu pale Pwani. Mwenzetu moja amezungumza hapa akasema kuwa kuna mkopo kutoka China. Ikiwa Serikali ya Kenya inataka kulipa mkopo huu wa SGR, basi sharti itambue kwamba SGR si ya watu wa Pwani pekee. Ni ya Kenya nzima. Haifai kugandamiza wafanyibiashara wa Mombasa ama Pwani kwa jumla kwa sababu ya kulipa mkopo."
}