GET /api/v0.1/hansard/entries/932768/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 932768,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/932768/?format=api",
    "text_counter": 450,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi kutoa maoni yangu kuhusu janga ambalo lilitokea kaunti ya West Pokot. West Pokot ni sehemu ya Kenya ambayo imekumbwa na shida nyingi. Kwanza, ningependa kutoa rambirambi zangu za dhati kwa watu wa West Pokot. Vile vile, ningependa kutoa rambi rambi kwa aliyekuwa Seneta na ambaye ni Gavana, Prof. John Lonyangapuo, kwa jitihada ambazo anafanya kusaidia watu wake. Nilisikitishwa sana na karibu machozi yanitoke nilivyo ona alivyokuwa akijieleza. Ni kama alikuwa analia. Alisema kwamba ameachiwa watu wa West Pokot ilhali hana uwezo. Hiyo ina maanisha Serikali haijatilia maanani watu wa West Pokot. Bi. Spika wa Muda, sehemu ikikumbwa na janga kama lile lililotokea West Pokot, Serikali inafaa kuingia kati mara moja. Serikali inafaa kutoa mikakati ili watu waone kwamba inaweza kuwasaidia, kuwatumikia, kuwapunguzia shida walizo nazo, na pia kuwatoa katika sehemu ambazo hazifai. Mito mingi imefurika na maeneo mengi yamekumbwa na mmomonyoko wa udongo. Hali hii imesababisha madhara makubwa. Kwa hivyo, Serikali, haswa Idara ya Utabiri wa Anga, inafaa kutahadharisha watu kutoka kwenye maeneo hatari ili kuepukana na majanga. Bi. Spika wa Muda, sio watu wa Kaunti ya Pokot Magharibi peke yao. Vile vile, watu wa Kaunti ya Kwale wamekumbwa na mafuriko. Watu wa Bunyala na Kaunti ya Kilifi pia hukumbwa na mafuriko. Miezi kadhaa iliyopita, kumekuwa na hali ya suitofahamu katika maeneo fulani ya Kaunti ya Kilifi ambapo watu walikuwa wakipelekewa chakula kupitia kwa ndege aina ya helikopta. Lazima sisi Wakenya tuzingatie mambo kama haya. Serikali yetu pia inafaa ihakikishe kuwa athari kama hizi zinazokumba Wakenya zinadhibitiwa kabla kutokea. Asante kwa kunipa muda huo. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}