GET /api/v0.1/hansard/entries/933286/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 933286,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/933286/?format=api",
"text_counter": 76,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii ili kuchangia taarifa hii kutoka kwa Sen. Prengei kuhusu Huduma Namba. Ni swala ambalo tulichangia na tukatoa mwelekeo wetu kwamba ni swala nzuri kulingana na maelezo tuliopata kutoka kwa Wizara. Tuliambiwa ukipata hii Huduma Namba, huhitaji kitambulisho chochote tena, kwa mfano, kuendesha gari, kusafiri, kupata NSSF na NHIF. Ile namba moja ingekupa huduma yeyote ungehitaji. La haula, ilivyo sasa ni kwamba katika kutoa huduma na kwa wale ambao wanahudumia Wakenya, kumekuwa na tatizo la kandarasi na yule ambaye anatoa huduma kuwa na maadili mema ili kuhakikisha ya kwamba malipo yametolewa jinsi yanavyofaa. Ninashukuru mstahiki Seneta wa Makueni ambaye amesema ya kwamba tulitumia kiima cha Kshs7 bilioni katika shughuli ya kupata huduma Namba. Hata hivyo, pesa ambazo zilitumiwa wakati wa zoezi hilo la kuwapa Wakenya huduma namba ni zaidi ni zaidi ya Kshs7 bilioni. Bw. Spika, ninasema hivyo kwa sababu kuna watu walipata mkopo kwa kusema kwamba wanafanya kazi ya Serikali ya kupeana Huduma Namba. Watu hawa walichukua mikopo kutoka madukani na watu binafsi na kuahidi kuwa wakilipwa na Serikali, watalipa mikopo hiyo. Kwa hivyo, ninafikiri watu wengi wanawadai wale waliotoa huduma ya kupeana Huduma Namba."
}