GET /api/v0.1/hansard/entries/933407/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 933407,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/933407/?format=api",
"text_counter": 197,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika. Kuambatana na Kifungu cha 48(1) cha Kanuni za Bunge la Seneti, nasimama kuomba Taarifa kutoka kwa Kamati ya Usalama wa Taifa, Ulinzi na Maswala ya Nchi za Nje kuhusu kupigwa risasi na kuuawa kwa mwendeshaji pikipiki, Leonard Komora, na Mwanajeshi wa Jeshi la Wanamaji katika Kambi ya Jeshi la Wanamaji la Mtongwe, Kaunti ya Mombasa, jana asubuhi tarehe 20 November, 2019. Katika Taarifa hiyo, Kamati inapaswa - (1) Kuelezea sababu za mwendesha boda boda huyo, kijana Leonard Komora, kupigwa risasi na kuuawa. (2) Kuelezea mbona mbinu m’badala hazikutumiwa kumthibiti kijana huyo, iwapo alikuwa tishio kwa usalama. (3) Kuelezea hali ya usalama baina ya raia wanaoishi karibu na kambi za kijeshi nchini kwa ujumla na wanajeshi, hasa kufuatia hali tete ya usalama baina ya wanajeshi na raia. (4) Kuelezea mikakati iliyowekwa na Serikali kupunguza na hata kuondoa hofu za wakazi dhidi ya wanajeshi kwa ujumla, na hususan wale wa Kambi ya Mtongwe, kwa kuwa tukio hili silo la kwanza. Hii ni kwa sababu mkaazi mwingine alipigwa risasi siku chache zilizopita. Asante, Bw. Spika."
}