GET /api/v0.1/hansard/entries/933422/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 933422,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/933422/?format=api",
"text_counter": 212,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13224,
"legal_name": "Golich Juma Wario",
"slug": "golich-juma-wario"
},
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda. Ningependa kuunga mkono Taarifa iliyotolewa na Seneta wa Mombasa, ya kwamba mtu wa boda boda ameuawa kiholela. Nilitoa arifa hapo mbeleni tukiwa Kitui, ya kwamba hawa watu watatu waliuawa sehemu ya Tana River na watu ambao walijitambulisha kama polisi. Na katika Taarifa yangu, nilipewa wiki mbili ili niweze kupata jawabu kuhusu wale waliofanya uhalifu huo. Lakini hivi sasa, bado tunaendelea kupata habari ya kwamba watu wa boda boda wanauawa. Vile vile tunaendelea kupata habari kwamba polisi pia waliwapiga vijana wa JKUAT . Tukio hili haswa lilinaswa dhahiri shahiri kwenye picha, likionyes polisi wakiwapiga mateke vijana, hata na wasichana pia. Kwa hivyo, naunga mkono Taarifa hii, na kama Seneti, tungependa Kamati ambayo ni ya Usalama wa Kitaifa, ambayo Sen. Sakaja ni Vice Chairman, itupatie habari hiyo ili tujue kwa nini polisi wanawanyanyasa watu katika nchi ya Kenya. Asante, Bi Spika wa Muda."
}