GET /api/v0.1/hansard/entries/934465/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 934465,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/934465/?format=api",
"text_counter": 824,
"type": "speech",
"speaker_name": "Trans Nzoia CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Janet Nangabo",
"speaker": {
"id": 1076,
"legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
"slug": "janet-nangabo-wanyama"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii kuunga mkono Mswada huu. Nataka kukubaliana na wenzangu ambao wamesema tuwe na sheria ya kuhakikisha kwamba wanaopewa kandarasi katika nchi yetu ya Kenya wanapata haki yao na wasinyanyaswe. Tulikuwa na shida sana na vijana wa National Youth Service kwa sababu hatukuwa na mikakati mwafaka wakati hao walikuwa wamechukua kandarasi ya kusema kwamba wanapeana bidhaa katika shirika hilo la Huduma kwa Vijana. Itakuwa vizuri iwapo tutakuwa na mikakati ya kuhakikisha kwamba iwapo unafanya biashara iwe ndogo au kubwa na uko na nafasi kwamba unalindwa vyema ukifanya biashara yako litakuwa jambo nzuri sana. Tukirudi mashinani, tunaona Serikali ya mashinani inawapatia watu kandarasi na huenda ikawa hawajafuata mikakati ya kujua kwamba mtu huyu anaweza kulima barabara hii au kufanya jambo hili. Inakuja kuonekana kwamba yule anapewa ni jamaa wa mtu fulani. Iwapo tutakuwa na sheria hii ya kuzuia na kuweka mikakati ya kusema kwamba kama umepewa nafasi ya kutengeneza kitu fulani, ni lazima mikakati fulani ifuatwe itakuwa vyema."
}