GET /api/v0.1/hansard/entries/934709/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 934709,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/934709/?format=api",
    "text_counter": 155,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante sana Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia taarifa iliyosomwa na Seneta wa Bungoma, Sen. Wetangula. Taarifa hii imeletwa hapa kwa wakati mwafaka kabisa. Serikali imeendeleza utepetevu katika kutetea hadhi ya inchi ya Kenya. Itakumbukwa kwamba tuna mzozo wa mipaka na Somalia na kesi hiyo iko katika korti ya kimataifa inayohusiana na mambo ya bahari. Vile vile, kule Vanga katika Kaunti ya Kwale, wavuvi wengi hushikwa na wanamgambo wa Tanzania wakati wanavua katika Bahari ya Hindi. Kwa hivyo Bw. Spika wa Muda, bahari ama nchi yetu si jambo la kuchezewa ovyo ovyo kwa sababu kuna Wakenya wengi ambao walimwaga damu na kutoa mali yao ili kupigania uhuru wa nchi hii. Kutoa ardhi kiholela kama ilivyofanywa huko Migingo si sawa. Bw. Spika wa Muda, utapata kwamba Wakenya wengi Migingo, haswa wavuvi, wamekuwa wakilalamika kuwa wanapokonywa mali, bidhaa na vifaa vyao vya uvuvi. Ikiwa tutaipatia Uganda nusu ya mamlaka, ina maana kwamba wale Wakenya wataendelea kuteseka ilhali wanaamini ya kuwa ni wananchi wa Kenya. Serikali ya Kenya ina jukumu la kuwalinda na kuwatetea kuhusiana na mali yao. Hili sio jambo la kudharauliwa. Ni jambo ambalo linahitaji Kamati husika kuaanda kwa upesi tukutane na Waziri ili swala hili litatuliwe haraka."
}