GET /api/v0.1/hansard/entries/934751/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 934751,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/934751/?format=api",
"text_counter": 197,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Taarifa iliyoletwa na Sen. Cherargei. Labda angetujulisha kama ana interest yoyote kwa sababu tunajua kwamba alimaliza masomo hivi karibuni. Hata hivyo, hiyo haitaathiri umuhimu wa Taarifa hii kwa sababu wanafunzi wengi humaliza masomo katika vyuo vikuu na kupata shida ya kuajiriwa na kufungua biashara. Kwa hivyo, si rahisi wao kulipa mikopo ya HELB ambayo inaendelea kuwasonga kama watu wanaotakikana kunyongwa. Itakumbukwa kwamba Serikali ilileta mikopo ya HELB ili kusaidia wanafunzi kusoma na pia Serikali iweze kupata watu walio na tajriba na ujuzi wa fani mbali mbali nchini. Si sawa kuwa-profile na kuweka picha zao magazetini na kuwakejeli kwa sababu ya kushindwa kulipa mikopo. Bw. Spika wa Muda, itakumbukwa kwamba Serikali imetupilia mbali mikopo ya sekta za sukari, majani chai na kahawa ambazo zilikuwa na mabilioni ya pesa ambazo wakulima walikopeshwa, ili wafanye biashara lakini biashara hizo hazikua. Sioni ni kwa nini wanafunzi waliofuzu wasisaidiwe kupata kazi. Wanafaa kupewa mikopo mingine waanzishe biashara ili wajiendeleze kimaisha na kulipia mikopo waliochukua. Si vyema kuwakejeli na kuwasukuma kwenye ukuta."
}