GET /api/v0.1/hansard/entries/934773/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 934773,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/934773/?format=api",
    "text_counter": 219,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ya kuchangia Taarifa hii. Kitu cha kwanza cha kusikitisha ni kwamba kutafuta kazi kwa mwanafunzi wakati amemaliza college ama chuo kikuu ni kibarua chenyewe.. Kwa hivyo, kuna vitu viwili; wale ambao wako katika shule wanasoma. Lakini tunajua kwamba wakimaliza kusoma katika vyuo vikuu, kibarua chao cha kwanza ni kutafuta kazi, ambayo ni kazi yenyewe. Sijui kama ninaweza kueleweka vizuri lakini nafikiria unaweza kunielewa vizuri. Nikisema zaidi ni kwamba yule mtoto akimaliza masomo yake na hapati kazi, inakuwa jukumu la wazazi wake kuendelea kumlisha ndani ya nyumba yao na huku anadaiwa deni na Serikali. Tukiweka mikakati ya kuzuia ufujaji wa pesa hizi kwa njia ya ufisadi, tutawasaidia watoto wetu ili waendelee na masomo yao hadi vyuo vikuu bila kutatizwa. Pia, tunatakiwa kuwa na mipango maalum kwa sababu tutakuwa na pesa za kuanzisha taaluma mbali mbali, ili waweze kupata kazi kulinganisha na elimu waliopata katika vyuo vikuu. Vile vile, tunaona janga la wanafunzi wa vyuo vikuu ambao wamemaliza masomo yao na hawana kazi. Siku hizi si guarantee ya kwamba ukimaliza shule, itakuwa kama ule wakati wetu; ya kwamba kazi inakungoja ndani ya ofisi. Kama ulisomea sheria, kazi ilikuwa inakungoja katika mahakama kuu ili upate kuajiriwa kama hakimu ama katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili upate kuajiriwa kama State Counsel . Wakati umekuwa mgumu. Vijana wengi ambao wamesomea taaluma mbali mbali wako barabarani na hiyo ni hatari kubwa ikiwa kijana huyo ambaye amesoma hana kazi na anajua kuwa atalipa deni la HELB wakati atapata kazi."
}