GET /api/v0.1/hansard/entries/934777/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 934777,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/934777/?format=api",
    "text_counter": 223,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Ninajua anaangalia runinga pale alipo na ninataka anisikize. Ikiwa wewe una uwezo afadhali ulipe mkopo huo mara moja badala ya kulipa pole pole ilhali watoto wa Kenya wako nyumbani bila kazi. Wengine wanadaiwa na wewe bado unalipa reja reja ilhali unaweza kulipa deni hilo mara moja. Ni jambo la kusikitisha kwamba watoto wetu sasa wameanza kujiingiza katika maswala mabovu mabovu ambayo yana madhara kwa Wakenya wenzao kama AlShabaab . Katika ufuo wa bahari, tunaona wengine wakivuta vitu ambavyo havitakikani kuvutwa. Kwa hivyo tunasema ya kwamba ikiwa hii HELB inaweza kupewa kama loan ya Serikali vile ambavyo vifaa vinavyotumika katika hospitali vimepeanwa halafu wao wanalipa baada ya miaka saba, kwa maana watu wanaenda zaidi ya miaka saba bila kazi. Haina haja mtu kama huyo akiwa hajalipa na hajapata kazi kulazimishwa kwamba siku ile atapata kazi alipe. Itakuwa muhimu pia kuona ya kwamba ikiwa hajaweza kulipa na imepita miaka mitano basi ninapendekeza mkopo huo uwe written off ili tusiendelee kuwajazia madeni watoto wetu wanaomaliza masomo katika vyuo vikuu. Asante, Bw. Spika wa Muda."
}