GET /api/v0.1/hansard/entries/934957/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 934957,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/934957/?format=api",
"text_counter": 403,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Tuliona vile mambo yalifanyika katika Mau Forest, hasa kule Kaunti ya Narok. Ilikuwa jambo muhimu sana kuzingatia kwamba mazingira yetu hapa Kenya yasiingiliwe kisha tuwe katika sintofahamu mbalimbali na kusababisha kukosa mvua kwa sababu ya ukataji miti katika Mau Forest. Ninampa kongole Seneta wa Kaunti ya Narok, Sen. Olekina, kwa sababu yeye alisimama kidete na Wakenya wakati mambo haya yalikuwa yakiendelea. Alisema kwaamba ikiwa unataka maji mazuri, mazingira bora, mvua na chakula, ni sharti tupande miti ndani ya Mlima wa Mau. Bi. Spika wa Muda, katika juhudi zake, ilimbidi Waziri wa Mazingira, Hon. Tobiko, aingilie kati na kupanda miti takribani milioni 10. Huyu ndugu yangu alileta vifaa ambavyo vilistaajabisha Wakenya sana na kupanda miti zaidi ya milioni 20. Siku hizi kuna teknolojia ya upazi wa miti. Unaweza kupanda miti kupitia kwa ndege kama unamwaga mbegu kutoka angani na miti itamea. Tunaisifu sana Serikali yetu kwa kuweka mazingira yetu mbele. Wale waliokuwa wamevamia msitu waliulizwa kuondoka huko pole pole na kwa hisani yao. Walifanya hivyo kwa hiari yao wenyewe. Hili ni ambo tunafurahia kwa sababu lilizungumziwa katika Ripoti hii. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}