GET /api/v0.1/hansard/entries/934958/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 934958,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/934958/?format=api",
"text_counter": 404,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Mwisho, kuna utendakazi na heshima ndani ya Bunge. Kuna wasichana kwa wavulana wanaoajiriwa ndani ya Bunge zetu za Jumuiya ya Madola. Wakati mwingine utapata kuna kukoseana heshima aidha kati ya wafanyikazi na Wabunge. Mambo haya yalijadiliwa katika mkutano wa Kampala. Sisi Wakenya, hasa Bunge la Seneti, tulifanya jambo muhimu sana kumtuma Sen. Faki, Seneta wa Kaunti ya Mombasa. Alienda kutuwakilisha katika mkutano huo muhimu ambao utaangalia na kuleta Ripoti ambayo itatekelezwa na Serikali yetu. Bi. Spika wa Muda, nilipokuwa Hakimu katika Mahakama Kuu, tuliangalia mambo ya wafanyikazi. Wafanyakazi wa Bunge na Waheshimiwa ambao wanafanya kazi pamoja, ni lazima wawe na heshima ili tusilete maonevu ya aina yoyote ambayo yanaweza kuleta madhara katika utendakazi."
}