GET /api/v0.1/hansard/entries/935917/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 935917,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/935917/?format=api",
    "text_counter": 38,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Zawadi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13176,
        "legal_name": "Christine Zawadi Gona",
        "slug": "christine-zawadi-gona"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika wa Muda, mimi pia ninachukuwa fursa hii kuwakaribisha MCAs wa Kaunti ya Trans Nzioa. Mimi nilikuwa MCA wa Kilifi County. Kwa hivyo, ninawakaribisha. Vile mheshimiwa Wetangula amesema hakuna mipaka kwa yale mambo binadamu anaweza kuyatekelez. Kesho ama kesho kutwa mnaweza kujipata mko hapa. Si maajabu, inawezekana. Ninataka kuwatia motisha ya kwamba, inawezekana. Bw. Spika wa Muda, nilipokuwa kwenye Bunge la Kaunti kulikuwa na mambo kama yale ambayo mmekuja kuangalia hapa. Inafaa mue makini sana wakati mnapoangalia kwa sababu tulipata kuna pesa fulani wanaingiza kwa akaunti kiholehole. Wanaweka mamilioni ya pesa katika hiyo akaunti kisha baadaye yule kibarua atatoa zile pesa, achukue kifungu kidogo, halafu zile zingine anapeana kwa wale wameweka hizo pesa. Kwa hivyo, mue makini wakati mnaangalia biashara zenu mnavyozifanya ili mhakikishe kwamba mambo kama hayo hayafanyiki. Hakuna cha ajabu hapa. Mambo ni yale yale ambayo mko nayo kwa kaunti yenu na kila mahali yanaweza kutokea. Zaidi ya yote, jipeni moyo, hasa viongozi waheshimiwa akina mama. Mtajipata mko Seneti ama mpiganie vitu vya wakilishi wa wanawake. Inawezekana."
}