GET /api/v0.1/hansard/entries/937036/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 937036,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/937036/?format=api",
"text_counter": 364,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taveta, JP",
"speaker_title": "Hon. (Dr.) Naomi Shaban",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "Ukweli ni kwamba saa nyingine utakuta wafanyikazi wa umma kwenye Serikali wanafanya kama utani kuwa wananchi hawatakikani kuhusishwa. Hivyo basi Kamati hii imefanya kazi nzuri ya kuhakikisha kuwa suala hili linatupiliwa mbali. Vile vile, ningependa kusema nimekuwa na wasiwasi. Tume hii ya kusimamia wafanyikazi wa umma inatakikana kusimamia wafanyikazi wote kwa ujumla. Tunajua kuna ngazi mbili hapa nchini. Kuna ngazi ya juu ambayo ni ya kitaifa na ngazi ya pili ni ile ya ugatuzi. Lakini wameshindwa kuangalia jinsi wataweza kuhakikisha kuwa wafanyikazi wa umma wote wanaangaliwa kupitia tume hii ambayo kwa kweli ni ya kitaifa. Hayo ndiyo masikitiko yangu makubwa lakini naunga mkono ripoti ya Kamati hii."
}