GET /api/v0.1/hansard/entries/937081/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 937081,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/937081/?format=api",
"text_counter": 409,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taveta, JP",
"speaker_title": "Hon. (Dr.) Naomi Shaban",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii ili nami pia nizungumzie suala hili kuhusu Hazina ya Vyama vya Kisiasa. Yangu kwanza ni kutoa shukrani kwa Kamati hii kwa kazi waliyofanya kuhakikisha kuwa mambo ya mtu mmoja kukaa mahali na kufanya uamuzi wa kuwa yeye atakuwa umma na kufanya uamuzi akiwa peke yake haiwezekani. Wabunge wote hapa nchini tumechaguliwa kuja kuhakikisha kuwa wananchi na hasa umma wanapata haki na tunalinda haki zao kupitia sheria zilivyo. Hivyo basi nakubaliana na Kamati kwamba Msajili Mkuu wa Vyama vya Kisiasa aweze kufuata sheria vile ilivyo na asiwe mtu anayefikiria kuwa anaweza kufanya kazi akiwa peke yake bila kufuata sheria na kuhakikisha kuwa wawakilishi wa wananchi na wananchi wanahusika katika masuala haya. Naunga mkono."
}