GET /api/v0.1/hansard/entries/93739/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 93739,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/93739/?format=api",
    "text_counter": 288,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ms. Leshomo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": "Ahsante, Madam Naibu Spika wa Muda. Mimi pia nataka kuchangia mambo ya ardhi. Ingekuwa muhimu kuongezea pesa mambo ya ardhi. Nafikiri sehemu zote zina shida; hasa shida za vyeti vya kumiliki mashamba. Kama pahali nimetoka, hakuna mtu ako na cheti cha kumiliki ardhi. Ningemwomba Waziri ajaribu kupanga semina ya kufunza watu mambo yanayohusu ardhi hasa kwa watu ambao wako chini ya miradi ya group ranches. Kwetu kuna group ranches na watu wana shida kubwa kupata title deeds. Pesa zinazohitajika ili watu wagawanyiwe ardhi ni nyingi sana. Watu wameshindwa kulipa. Kwa hivyo, mimi pia ningeomba Waziri ajaribu kufanya semina katika sehemu zote kama vile Turkana, Pokot, Samburu na North Horr. Watu wanafaa kufudishwa maana ya group ranches na title deeds. Kuhusu title deeds, kuna wachache wana mashamba katika sehemu hizo. Lakini utakuta mtu anaingia katika shamba la mwenzake na mwenye shamba anashindwa atatumia sheria gani kumtoa hapo."
}