GET /api/v0.1/hansard/entries/937415/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 937415,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/937415/?format=api",
"text_counter": 313,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Obo",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": " Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nimeamka kuunga mkono Mswada huu. Kama unavyojua, uongozi huja na kwenda. Leo tuko hapa na siku nyingine tutakuwa kwingine. Lakini maisha huwa magumu kule nje baada ya kuja hapa. Hii ni kwa sababu ukishakuwa kiongozi na kuja hapa Bungeni, hata wakati uko nyumbani, wananchi wanakufuata hata kama hawakukuunga mkono. Lakini wao huja kukwambia shida zao na kusema wamejuta. Lakini kama wewe ni kiongozi, lazima uwe pale kuwasaidia kwa matatizo yao."
}