GET /api/v0.1/hansard/entries/937430/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 937430,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/937430/?format=api",
    "text_counter": 328,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Mimi pia nachukua nafasi hii kumuunga mkono kiongozi kutoka chama changu, Mhe. Mbadi, kwa sababu ya Mswada huu. Mswada huu ni muhimu haswa tukizingatia Wabunge ambao walichaguliwa mwaka wa 1984. Wakati huo walikuwa wanapata mishahara duni na haba. Pia hawakuwa na limbikizi ambayo ingeweza kuwawezesha kufanya miradi fulani ya kujikimu katika maisha yao. Mbunge yeyote ambaye anachaguliwa katika taifa la Kenya ni Mkenya kama Mkenya mwingine ambaye hufanya kazi na, wakati amestaafu, akaweza kupata pesa hii ya uzeeni. Iwapo sisi viongozi kama hawa ambao pia siku moja tutakuwa Wabunge wastaafu hatutawafikiria katika maisha yao, itakuwa makosa makubwa sana. Tumeona viongozi wengi sana ambao wametoka katika Bunge hili. Hata anapoingia katika jamii na kutafuta kazi katika taasisi za Serikali au za kibinafsi, inakuwa vigumu kwao kuandikwa kazi kwa sababu kwanza watu wanakuchukulia wewe kuwa mtu wa siasa na wanasema pengine unapoingia katika taasisi yao, utaleta siasa na fitina. Hivyo basi, ni vigumu sana kupata Mbunge mstaafu ameandikwa kazi tena katika sekta ya umma au ya kibinafsi. Ndiposa tunasema viongozi kama hawa lazima wawekewe pesa hizi ambazo Bunge hili leo tunapitisha Mswada. Pesa hizi wakizipata, tunajua wengi wana familia na wanasomesha. Kuna Wabunge ambao wameingia katika Bunge hili wakiwa wachanga sana. Nikifikiria siku za nyuma, nafikiria kama Mhe. Khaniri wakati ule akiingia Bungeni alikuwa kiongozi mwenye umri wa chini ya miaka 30. Nafikiri alikuwa kama miaka 26. Kwa hivyo, ukiona kiongozi ameingia hapa akiwa na The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}