GET /api/v0.1/hansard/entries/937431/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 937431,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/937431/?format=api",
    "text_counter": 329,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "miaka 20 au 25, amekaa pengine mihula miwili na akatoka akiwa na miaka 30, mtu huyo hawezi kuandikwa kazi mahali pengine. Halafu awe hana pesa ambazo zinaweza kumkimu kimaisha, inakuwa matatizo sana. Najua pengine watu wanauliza kwa nini tunapitisha Mswada huu na labda pengine kutakuwa na mambo ya pesa kuongeza bajeti ya kuwakimu katika suala kama hili, lakini nataka niseme, kupitia Katiba yetu, tunajua Wakenya tuna usawa na tuna haki kwa mujibu wa Katiba. Kwa hivyo, kiongozi ambaye amewakilisha taifa la Kenya kupitia Bunge pia ana haki kama Mkenya mwingine yeyote ambaye amewakilisha taifa katika taasisi za umma au za Serikali. Kwa hivyo, hawa wote lazima wapate haki zao za kimsingi na waweze kuendelea. Katika siku za hivi majuzi, tumeona kuna mkurupuko wa maradhi mengi sana kama saratani. Wakenya wengi sana wanashikwa na maradhi ya saratani na haswa viongozi kutokana na kwamba wanakuwa na mambo mengi sana ambayo wamepitia katika maisha ya kazi zao za kisiasa. Wamekuwa na misukosuko mingi katika kazi za kisiasa. Wengi utawapata wanashikwa na maradhi pengine ya kisukari na saratani ambayo yanahitaji mtu kuwa na fedha au kuwa na kitita cha pesa ambacho kinaweza kumkimu katika mambo ya kiafya. Kwa hivyo, iwapo hatutaweza kuwaangalia, hilo litakuwa tatizo nyeti sana. Nataka kuwaambia Wabunge wenzangu; sisi pia njia ni hiyo hiyo kwa sababu hatutakaa milele katika Bunge hili. Watu watasema wanakupenda, watakuchagua na itafika wakati watasinywa na wewe na waseme ni wakati pia wewe unapaswa umpishe mwingine. Kwa hivyo, kama tutaweka mikakati ya usawa, tutapunguza shida nyingi za jamii kwa sababu yule Mbunge ana familia ambayo inamsimamia. Vile vile, unapokuwa Mbunge, hata unapostaafu au unapokosa kiti, bado unabeba taji kwamba wewe ni Mheshimiwa. Hivyo basi, watu wana matarajio mengi sana kutoka kwako na utakuta hata kila mahali unapokwenda kama ni mazishini au kwenye sherehe za kijamii, basi watu wanakuwa na tamaa nyingi sana kwamba Mheshimiwa ameingia na anaweza kutusaidia katika jambo fulani. Kwa hivyo, kiongozi huyu huwa ameingia katika anga zingine na hesabu nyingine ambapo kama hatakuwa na pesa ambazo zinamsaidia, ataishi maisha ya uchochole. Wakati anaishi maisha ya uchochole, kutatokea mambo mengi sana. Hata unaona mara nyingi sana viongozi wengine waliokuwa nyuma wanatamautishwa au kuwa na shida nyingi sana mpaka unasikia ameamua kuunda jopo fulani ili kusudi ajitengenezee ajira. Inakuwa bado ni changamoto. Serikali yetu ya Kenya katika mikakati yake - haswa kuhusiana na bajeti… Hizi hazitakuwa pesa nyingi sana za kuwakimu viongozi hawa ambao wamepigania taifa la Kenya. Wamejenga taifa. Ukiwa mwakilishi katika Bunge la Kitaifa, umejenga taifa kwa njia nyingi sana. Kwanza, umetengeneza zile sheria ambazo zimebuni mambo mengi sana kuongoza taifa la Kenya. Pili, umewakilisha matakwa ya Wakenya wengi ambapo bila ya kufanya mambo kama hayo, Kenya haingeweza kusonga mbele. Kwa hivyo, hawa ni watu muhimu sana. Mheshimiwa Mbadi ambaye ni kiongozi katika chama cha chungwa, alifikiria jambo la msingi sana kusema ya kwamba lazima Wabunge hawa waongezewe pesa hizo. Ikiwa hizo pesa zimeongezwa, kusiwe na kizungumkuti ya kwamba pesa hizo ziko lakini Mbunge huyu ambaye amestaafu ama amekosa kuingia kwenye mamlaka tena anazungushwa. Inakuwa kama ni ule mchezo wa paka mshike panya. Hayo ni mambo tumeyaona hata kwa zile taasisi nyingine za Kiserikali. Mambo ya pensheni yamekuwa na shida. Wazee wengi The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}