GET /api/v0.1/hansard/entries/937432/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 937432,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/937432/?format=api",
    "text_counter": 330,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "wamefariki bila kuonja utamu ama kupata asali ya hizo pesa za pensheni. Kumekuwa pia na mambo ya ufisadi sana katika mambo ya pensheni. Iwapo sisi tunaweka Mswada kama huu, lazima mikakati na miundo msingi iwekwe sambamba kuhakikisha ya kwamba fedha hizi zitawafikia kwa wakati unaofaa. Tukisema wakati unaofaa ni aweze kupata fedha zile ikifika mwisho wa mwezi ama pengine ikizidi sana, iwe ni tarehe tano ili aweze kukimu maisha yake. Ikiwa itakuwa tu ni mazungumzo baada ya habari, tumetengeza sheria na zile pesa pengine zimetengwa lakini inakuwa, “Njoo leo, njoo kesho, rudi, ama sasa hivi hakuna pesa tutatoa wakati mwingine”, basi lile donda sugu la kutaka kumaliza umasikini na kusaidia kuondoa uchochole kwa viongozi hatutaweza kulikimu. Bunge hili limefanya maamuzi mengi sana ambayo ni mazuri sana na yako sambamba na mataifa yaliyostawi. Katika mataifa yaliyostawi mengi, mtu ambaye amekuwa kiongozi na kujenga taifa lake huwa anapewa kitu kile kwa Kiingereza tunasema a certain package, yaani huwa kuna malimbikizi fulani ambayo yametengewa ili kumuwezesha kiongozi yule aweze kujipanga katika maisha yake ndio asionekane ya kwamba alikuwa ni mtu tu wa kawaida. Kuitwa “Mheshimiwa” si rahisi. Sisi sote tumeingia katika nyanja za siasa. Tumepiga siasa na tunajua siasa ni nini. Tunajua zile changamoto. Iwapo tumeng’ang’ana, tumesimama kidete na taifa letu mpaka tukaingia katika Bunge hili, iwapo tutatoka lazima tutoke na heshima. Tupewe ile heshima yetu kama viongozi wanavyopewa heshima wafanyikazi wengine wa Taifa la Kenya kwa sababu sisi sote ni Wakenya na tuna haki zetu za kimsingi. Ni haki kwa taifa kuangalia ya kwamba Mkenya kweli ana makao, anapata chakula na ana masomo. Hivyo basi, vizazi na vizazi vya viongozi hawa wataweza kupata masuala yote haya ambayo yamewekwa katika Katiba yetu, na sisi Wabunge wenyewe ndio tumepitisha Katiba kama hiyo. Naunga mkono Mswada huu. Nataka kuwaambia wenzangu nimefurahi kuwa tangu tulipoanza Mswada huu, sijasikia hata kiongozi mmoja ambaye amepinga, ijapokuwa kuna wale ambao wanataka kuleta marekebisho machache ili kuboresha Mswada huu. Cha msingi, nitaomba, tuboreshe kwa njia ya kujenga zaidi ili watu wale wafaidike zaidi. Tusilete marekebisho ambayo yatadunisha Mswada huu na kufanya sasa tusiweze…."
}