GET /api/v0.1/hansard/entries/937487/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 937487,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/937487/?format=api",
"text_counter": 35,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Mheshimiwa Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia maombi ya Sen. Cherargei. Kwanza, ninampongeza Sen. Cherargei kwa kuleta maombi haya katika Bunge la Seneti. Juzi tulikuwa safari Tana River ambapo tuliona wananchi walivyokuwa wakipata shida kwa sababu ya kusimamishwa kazi kwa madaktari pamoja na wauguzi. Wagonjwa wengi waliokuwa Hospitali Kuu ya Hola, walikuwa hawana huduma kwa sababu madaktari na clinical officers wote walikuwa kwenye mgomo. Mhe. Spika, kwa hakika sijui kuna shida gani kwa sababu hata amri za mahakama za wafanyi kazi haziheshimiwi. Hiyo inaonyeshwa kwamba, tunapoteza mwelekeo. Ikiwa mahakama itatoa amri na isitekelezwe inamaana kuwa, tunapuuza tasisisi ambazo zinaweza kutusaidia kutatua mizozo yetu. Mhe. Spika, ninampongeza Mhe. Cherargei kwa maombi haya. Tunaiomba Kamati husika isizembee katika swala hili. Tunafaa tupate utatuzi wa haraka kwa sababu wananchi wengi ambao wanategemea huduma za madaktari hawa, wanapata shida katika kaunti zetu. Asante Mhe. Spika."
}