GET /api/v0.1/hansard/entries/937774/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 937774,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/937774/?format=api",
    "text_counter": 322,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Mswada wa Sheria ya Mbinu M’badala za Kutatua Mizozo ya Kibiashara na ya Kijamii. Kwanza, ningependa kumpongeza Sen. Kasanga, kwa kutayarisha Mswada huu; na pia kwa hisia nzito ambazo amezionyesha kwa kutaka kupitishwa Mswada huu. Namuunga mkono na kumshauri kwamba aendelee na moyo huo huo, ili aweze kuweka alama katika kazi yake katika Bunge hili la Seneti. Pili, maswala ya kutatua mizozo kwa mbinu mbadala sio maswala ya sasa; bali yamekuwa nasi kwa muda mrefu katika nchi yetu ya Kenya. Kabla ya kuja Mkoloni, kila jamii Kenya ilikuwa na mbinu zake za kutatua mizozo. Kuna wengine ambao walikuwa wanatumia viapo. Wengine walikuwa wanachimba shimo, halafu unaambiwa ukiruka shimo hili, basi itakuwa haukufanya makossa. Iwapo utatumbukia katika hilo shimo, basi utakuwa umefanya makosa. Kwa hivyo, kila jamii ilikuwa na mbinu zake m’badala za kutatua mizozo yake. Walipokuja Wakoloni, walituletea mahakama za kisasa, ambazo zilitumika kama njia ya sawa sawa ya kuamua matatizo na mizozo ambayo tulikuwa nayo, kama jamii; na pia baina ya Serikali na wananchi. Lakini jinsi muda unavyokwenda, tumeona kwamba mahakama zimelemewa na kazi hii. Kwanza kabisa, ningependa kupongeza mahakama kwa kujaribu kupunguza mlumbiko wa kesi. Lakini utapata pia kwamba kwa sababu ya upungufu wa rasilimali za fedha, za binadamu na pia majengo, utapata kwamba mahakama nyingi zinakaa na kesi kwa muda mrefu, hadi baadhi ya wahusika wanafariki dunia kabla ya matatizo yao kutatuliwa. Kuna haja ya kuangalia mbinu mbadala ya kuweza kutatua mizozo kama hii. Ndivyo Katiba yetu, katika Kifungu cha 159(2), kinasema kwamba katika kutekeleza haki, mbinu za kitamaduni za kutatua mizozo zitatumika ili kuhakikisha kwamba haki inapatikana katika mahakama zetu. Kifungu cha 48 pia kimetilia mkazo kwamba kila mtu"
}