GET /api/v0.1/hansard/entries/937780/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 937780,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/937780/?format=api",
"text_counter": 328,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "inafanyika hivi sasa, kwa sababu, ukienda katika sehemu nyingi katika kaunti zetu, kwa mfano kule Mombasa, kuna sehemu ambayo iko katika eneo la Miritini katika Jomvu Constituency, ambapo kila Jumapili, watu walio na matatizo ya kijamii – kama matatizo ya ndoa na matatizo madogo madogo kama ya mipaka – wanakuja kukaa chini na kuna wazee ambao wanakuja kuyatatua matatizo kama hayo. Kwa hiyo, Sheria hii, itaweza kusaidia kuleta kutambulika kwa kazi ambazo zinafanyika kwa wale ambao tayari wanafanya kitamaduni, na vile vile watu wengine ambao wameingia katika taaluma hii kwa sasa. Kwa mfano hivi sasa, kuna vyama tofauti ambavyo vimeundwa ili kushughulikia masuala ya usuluhishi. Hivi vyama vyote vinataka sheria ambayo itahakikisha kwamba wanaweza kufanya kazi yao bila kupata matatizo. Kwa hivyo, lazima tutumie mbinu za jadi za upatanishi sasa. Hii ni kwa sababu umefika wakati ambao tunaona kwamba mbinu za kisasa, kama vile mahakama, zimekorogeka, na wananchi hawawezi kupata haki kwa haraka invyotakikana. Lakini ninapozungumzia mbinu za kijadi, simaanishi zile mbinu ambazo zilikuwa zinatumika wakati wa nyuma. Kwa mfano, kule Kilifi, kulikuwa kuna mahali ambapo watu wanapewa shoka la moto. Kwa mfano, ukishtakiwa kwamba umeiba na umekataa kukubali hayo mashtaka, unapelekwa kwa mahakama ile ya kitamaduni, na unaambiwa, “Shika shoka hili la moto; kama umefanya makosa, shoka litakuchoma; kama haukufanya makosa, shoka halitakuchoma.” Kwa hivyo, hatuwezi kutumia mbinu kama hizo katika karne hii ya ishirini na moja. Vile vile, tumesema kwamba sheria hii inatoa fursa ya kuandikishwa kwa wanaotekeleza taaluma hii ya usuluhishi na taaluma ya upatanishi. Hii ni kwa sababu kwa sasa, wengi wao hawajakuwa na mwongozo ambao utawapatia nafasi ya kuwatayarisha. Kama alivyotangulia kusema Sen. Kasanga ni kwamba kitu muhimu ambacho tunafaa kuangalia, ni kwamba wale ambao watakuwa wanafanya kazi hizi za upatanishi na usuluhishi, watakuwa ni watu waadilifu. Tabia zao na hulka zao zinafaa ziwe sawa kabisa na wananchi ama jamii inawakubali kwamba hawa wanafaa kuwa wasuluhishi. Naibu Spika, tumeona pia kwamba usuluhisho na upatanishi zote zinaweza kutumika kusaidia kupunguza gharama za mahakamani. Utapata kwamba katika mizozo mingi inayokwenda kotini, gharama za wakili, koti na labda za mashahidi zinakuwa"
}