GET /api/v0.1/hansard/entries/937782/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 937782,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/937782/?format=api",
    "text_counter": 330,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "nyingi, kiasi ambacho Wakenya hawawezi kupeleka kesi zao mahakamani ili zitatuliwe. Kwa hivyo, upatanishi na usuluhishi utasaidia pakubwa kupunguza gharama ya kupata haki katika jamii yetu. Kfungu cha nne, yaani Part 4, kinatoa fursa kwa wale ambao labda hawakuweza kuelewana, kwenda mahakamani kutatuliwa tatizo lao, baada ya kushindwa kutatua tatizo hilo kupitia kwa upatanisho na usuluhishi. Hii sheria inaleta mwongozo, kwamba kabla ya kwenda mahakamani, watu waweze kupewa fursa ili wakae chini, wajaribu kutatua mzozo ule bila ya kwenda kwa mahakama, kama nafasi ya kwanza ya kujaribu kutatua tatizo hilo. Sheria hii inatoa nafasi ya kukaa chini kabla ya kwenda mahakamani; na baaadaye, ikiwa hawataweza kuelewana, vile vile mwisho wanaweza kwenda mahakamani ili kutatua tatizo hilo. Bw. Naibu Spika, sheria hii pia inatoa fursa ya kwamba yale makubaliano ambayo yataweza kupatikana, yataandikishwa na kupelekwa mahakamani kama makubaliano ambayo yamekubaliwa katika mzozo ule. Hii itasaidia pakubwa kuona kwamba haki inatendeka. Mara nyingi, makubaliano yanayofanywa katika vikao vya wazee huishia kwa chifu. Chifu anaposhindwa kuyatekeleza, mara nyingi huyapeleka kwa polisi, ilhali swala lile si la kupelekwa kwa polisi, bali ni swala la kupelekwa mahakamani kuhakikisha kwamba kunapatikana makubaliano. Bw. Naibu Spika, fursa hii ya kuandikisha makubaliano yale na kuyapeleka mahakamani itasaidia pakubwa kuhakikisha kwamba haki inatendeka. Ile amri ya mahakama itakuwa rahisi kutekelezwa kuliko zile ambazo zinafanyika hivi sasa. Sheria hii inatoa fursa ya kuhakikisha kwamba mbinu mpya za kutatua mizozo, suluhisho na upatanishi zinatumika katika kutatua mizozo kama hii. Kuna taasisi kadhaa ambazo zimeanzishwa nchini ambazo zinatoa mafunzo ya taaluma ya upatanishi na usuluhisho. Hizi taasisi zitasaidia pakubwa kuhakikisha kwamba watu wanapata mbinu mpya ambazo zitasaidia kutatua matatizo hayo. Pia, sheria hii inatoa mwongozo kwamba wale ambao wataweza kufanya upatanisho na suluhisho kuandika ripoti yao, ambayo itaashiria ya kwamba ule mzozo umetatuliwa ama haujatatuliwa, na kupelekwa mahali pengine. Bw. Naibu Spika, sheria hii itasaidia pakubwa kupunguza malimbukizi ya kesi, na gharama ambazo ziko mahakamani. Kama ni tatizo la biashara na mahakama imechelewa kutoa uamuzi, ina maana kwamba pesa za mwekezaji zitafungwa katika mzozo ule, na vile vile hatutaweza kukuza uchumi wetu vile inavyotakikana. Ningependa kutaadharisha kwamba kuna maswala mengine ambayo yanahusiana na mipaka. Kwa mfano swala la wasichana kubakwa. Wengine wangependa kupeleka kesi hizi mbele ya wazee ili walitatue; na wengine watasema kuwa lipelekwe mahakamani ili polisi waweze kulishughulikia. Maswala kama haya ni lazima yaangaliwe, kwa sababu mara nyingi haki haipatikani. Juzi, tulipozuru Gereza la Kitui, tulipata kwamba vijana wengi ambao wameekwa ndani, wameekwa kwa makosa ya kusingiziwa, kwamba walibaka, na wale ambao walidaiwa kubakwa wako nje. Wameendelea na maisha yao na labda wameolewa na watu wengine, wakati wale wanatumikia vifungo na kuzuiliwa katika rumande kwa maswala ambayo yangeweza kutatuliwa."
}